SARPS

MFUMO WA KUCHAKATA MATOKEO YA KITAALUMA NA RIPOTI ZA WANAFUNZI (SARPS)
Katika mambo yanayoleta changamoto kubwa kwa walimu katika shule nyingi tangu muda mrefu ni kuandaa ripoti za kitaaluma za wanafunzi. Walimu wa madarasa na wataaluma hujikuta wakiangukia katika wakati mgumu sana mara tu baada ya kusahihisha kazi walizofanya wanafunzi kwenye mitihani yao, iwe ni mitihani ya kila mwezi au ya robo muhula au nusu muhula au ya kumaliza mwaka. Imefikia hatua hata ripoti zenyewe hazitolewi kwa wakati kwa sababu ya kutumia muda mrefu kuchakata matokeo na ripoti za wanafunzi ili kupata nani ameshika nafasi gani kwa wastani na daraja gani kati ya wanafunzi wangapi na mambo mengine mengi ambayo hayawezi kufikiwa lakini ni muhimu sana. Changamoto hizi zinapelekea kukwama kwa baadhi ya mambo ambayo ni muhimu sana Mfano
  • Ni vigumu kufanya tathimini halisi ya taaluma kwa mitihani husika?
  • Ni vigumu kufanya ulinganifu wa kitaaluma baina ya muda na muda au mtihani mmoja na mwingine
  • Ni vigumu kutoa ripoti kwa wanafunzi kwa wakati na kuwafikia wazazi kwa wakati husasani wanapoondoka kwenda likizo n.k
  • Ni vigumu kwa wataaluma au walimu wa madarasa kupata matokea ya pamoja ya wanafunzi (mkeka) kwa matumizi ya ofisi, mfano matokeo yanayoonesha Alama tu, au Madaraja tu, au Alama na Madaraja kwa kila mwanafunzi, au Mukhutasari wa ufaulu wa kila somo na mengine mengi ambayo ni muhimu kiofisi
Kukua kwa Sayansi na Teknologia sasa kumeweza kurahisisha mambo mengi sana ambayo yalikuwa ni sehemu ya kukwamisha mengi ambayo wengi wangependa kuyafanya. Pamoja na hayo yote Matumizi ya Kompyuta mashuleni yamekuwa ni sehemu ya kutatua baadhi ya changamoto
Baadhi ya shule sasa zimeshafanikiwa kwa kiasi kikubwa kujikwamua na changamoto kama hizi kwa kutengeneza mifumo mbalimbali ya kuendeshea mambo ya kishule kama taaluma, fedha, utawala n.k
Kutokana na kuona tatizo hili wanalopata walimu wengi katika shule ambazo bado hazijapata kujikomboa na changamoto za namna hii, tumekuletea mifumo  ambayo itawasaidia walimu sasa kutoa ripoti za wanafunzi wao kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwataumia wazazi/walezi taarifa za maendeleo ya watoto wale kwa njia ya SMS kwa kutumia Software ya DRPU Bulk SmS bila mtandao (internet). Lakini pia wanaweza kupata  mengi ambayo ni vigumu kwao kupata katika tathimini mbalimbali za kitaaluma. Mifumo hii imetengenezwa kwa Kutumia Programu ya Excel.
Mifumo ipo ya aina tatu, mmoja ni kwa ajili ya shule za msingi, wa pili kwa ajili ya shule zenye kidato cha 1-4 na mwingine ni kwa zile shule za Kidato cha 5-6. Pata mfumo wako wa halali kwa ajili ya shule yako mapema kwa gharana nafuu ili ufanye tathimini na mambo yako ya kitaaluma kwa wakati.
Mifumo yetu ya SARPS imegawanywa katika matoleo mawili ambayo ni toleo la kwanza (Old Version) na Toleo la Pili (New Version) ili kumrahisishia mhitaji kupata mfumo kwa hali yoyote ya kiuchumi aliyonayo wakati huo. Gharama za mfumo wa toleo la kwanza ni ndogo zaidi kulinganisha na zile gharama za toleo jipya. Angalia machapisho ya toleo la kwanza na toleo la pili kufahamu zaidi
SARPS
PIMARY
SARPS
O LEVEL
 
SARPS
A LEVEL

Angalia Gharama

No comments:

Post a Comment